Vyama vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vimeyakataa matokeo ya awali ya uchaguzi wa Novemba 28 yanayoonesha Rais Kabila anaongoza
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenyeji wake wa China Rais Xi Jinping, waahidi kuanza zama mpya ya ushirikiano. Serikali ya Sudan Kusini yaafikiana nchini Kenya na makundi ya uasi kukomesha vurugu na uhasama. Korea Kaskazini yakanusha tuhuma za kubadilishana silaha na Urusi.
Hali ya Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico aliyepigwa risasi jana Jumatano sasa imeimarika. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hali ya Utulivu sasa imeanza kurejea katika mkoa wa Kharkiv. Na Marekani ina matumaini kuwa Angola itasaidia kupunguza hali ya mvutano kati ya Rwanda na DRC.
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Mei 15, 2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.