Deutsche Welle:Harakati za Namibia za kutaka kuzuia Burkina Faso ifurushwe kucheza michuano ya bara Afrika mwaka huu kuanza mahakamani kesho.
Klabu ya Al Hilal Benghazi ya Libya imetoka sare ya 1-1 na Rayon Sports ya Rwanda katika mchuano wa Kombe la shirikisho barani Afrika. Klabu hiyo ya Libya itasalia Kigali kwa wiki moja wakisubiri mchezo wa marudiano utakaochezwa Septemba 30. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Christopher Karenzi kutoka Kigali, Rwanda.
Shirika la mazingira la Ujerumani “Sports for Future” limekosoa uamuzi wa kuandaliwa kwa michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2030 katika nchi sita badala ya mabara matatu.
Wekundu wa Msimbazi Simba waparamia kileleni mwa Ligi kuu Tanzania bara, huku timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa stars ikijinoa kwa mechi ya kufuzu kwa michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN. Sikiliza ripoti ya Sports Lady Naomi William kutoka Dar es Salaam. (Pichani)