Vurugu zimesababisha vifo vya watu kadhaa mkoani Arusha nchini Tanzania kufuatia mvutano wa kisiasa kati ya chama tawala CCM na upinzani Chadema
Vita vinavyoendelea katika Ukanda wa Gaza vimeibua mijadala nchini Malaysia na maeneo mengine ya Kusini-mashariki mwa bara la Asia kuhusu kile kinachotajwa kuwa ni kuporomoka kwa maadili katika nchi za Magharibi.
Ulimwengu unaadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari, Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa uandishi wa Habari na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. Ujumbe huu unalenga nini katika tasnia ya wanahabari na jamii kwa jumla? Saumu Njama amezungumza na Salome Kitomari Mwenyekiti wa taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA
Chama tawala nchini Uingereza, Conservative, kimeshindwa kutetea kiti cha ubunge mbele ya chama kikuu cha upinzani cha Labour, wakati taifa hilo likisubiri matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa