Deutsche Welle: Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeahirisha utangazaji wa matokeo ya uchaguzi hadi Alhamis, huku usalama ukiimarishwa.
Baada ya zaidi ya miaka 20, Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO umeanza kuondoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mamlaka za nchi hiyo. Baadhi ya raia mashariki mwa Kongo wahofia kuondoka kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.
Shambulizi la anga limewaua karibu watu tisa hii leo, miongoni mwao watoto saba katika kambi ya wakimbizi wa ndani mashariki mwa mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Idadi kubwa ya Polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliotumwa mwishoni mwa mwezi Februari Mashariki mwa nchi hiyo ili kuchukua nafasi ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, wanakabiliwa na hali ngumu.