Timu ya kandanda ya Ujerumani, Bayern Munich, imemtimua kocha wake, Louis van Gaal, huku ikiwa imebakisha mechi tano kumaliza msimu huu wa ligi.
Ukraine imesema hii leo kuwa imezima mashambulizi 55 ya Urusi katika eneo la mashariki la Donetsk, siku moja baada ya kukiri kuwa hali ni mbaya zaidi katika mstari wa mbele wa vita.
Viongozi wa Afrika wanayataka mataifa tajiri kujitolea kuchangia mfuko wa Benki ya Dunia kwa ustawi wa mataifa yanayoendelea na kuyawezesha kukabiliana na jinamizi la mabadiliko ya hali ya hewa.
Waziri Kiongozi wa Scotland Humza Yousaf amejiuzulu.Hatua ya kiongozi huyo imejiri zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuchukua nafasi hiyo.