Bayern Munich imerejea kileleni mwa ligi ya Ujerumani Bundesliga baada ya kuishinda VFB Stuttgart kwa mabao 2-1 jana.
Umoja wa Mataifa umeziomba Israel na Hamas kutopoteza fursa ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano+++Marekani imetoa wito kwa Rwanda iviadhibu vikosi vilivyohusika kufanya shambulizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Kenya na Somalia zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baada ya waziri mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre kufanya ziara rasmi na kupokelewa na naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitolea wito Israel na Hamas kuongeza juhudi ili kufikiwe mkataba wa amani.