DW:Damu yaendelea kumwagika huko Syria huku mkuu wa kamisheni ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navy Pillay aulaumu umoja huo kwa kushindwa kukomesha ghasia Syria.
Israel imekuwa ikiishambulia Syria kwa siri kwa muda mrefu, ikijaribu kuvishambulia vikosi vinavyoipinga ili kuvizuia visiwe na nguvu na wataalamu wana hofu kuwa mzozo wa Gaza, huenda ukafanya mambo kuwa mabaya zaidi.
Shirika la uangalizi wa vita nchini Syria limesema watu 12 wameuwawa Kusini mwa mkoa wa Daraa katika vurugu zilizosababishwa na mripuko uliotokea hapo jana na kusababisha mauaji ya kundi moja la watoto.
Israel iliendeleza mashambulizi zaidi katika Ukanda wa Gaza siku ya Alhamisi (Aprili 18), wakati mataifa yenye nguvu duniani yakihofia kuwa huenda ikaishambulia tena Iran baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi.