Deutsche Welle: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemuonya Rais Bashar al- Assad wa Syria dhidi ya ukandamizaji kwa raia kuwa hauna mwisho mwema.
Idadi ya waliofariki baada ya shambulizi la Israel nchini Lebanon imefikia watu watatu na watu wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya. Haya ni kwa mujibu wa vyanzo nchini Lebanon.
Kesi dhidi ya mwanamume mmoja raia wa Syria mwenye umri wa miaka 47 imeanza kusikizwa leo mjini Hamburg, kaskazini mwa Ujerumani kuhusiana na uwezekano wa kufanyika uhalifu wa kivita uliofanywa na wanamgambo.
Shirika la uangalizi wa vita nchini Syria limesema watu 12 wameuwawa Kusini mwa mkoa wa Daraa katika vurugu zilizosababishwa na mripuko uliotokea hapo jana na kusababisha mauaji ya kundi moja la watoto.