Deutsche Welle: Mechi za fainali za Mpira ya Miguu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika zinaanza kesho, ambapo mara hii zinafanyika Gabon na Equatorial Guinea.
Marekani itatoa msaada wa karibu dola milioni 55 kushughulikia mzozo mbaya wa kibinadamu nchini Burkina Faso. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu ofisi ya Misaada ya Kitutu ya Marekani, Samantha Power.
Kwa mara ya kwanza, Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemsifu waziwazi mwanawe, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, akimtaja kuwa mzalendo aliye na azma ya kuboresha jeshi la Uganda, akionekana kumpigia debe kumrithi.
Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameikosoa Ulaya na kampuni za kimataifa kwa kujihusisha na biashara ya 'madini yenye damu,' huku akimtaja Rais Paul Kagame wa Rwanda kama mhalifu dhidi ya Kongo.