Ghasia zimeendelea nchini Ugiriki baada ya mamia ya vijana wanaopinga mipango ya serikali ya kubana matumizi kupambana na polisi.
Ni kwa nini mfungwa asalie gerezani hata baada ya kumaliza kifungo chake? Ndilo swali ambalo makala ya Mbiu ya Mnyonge inaangazia kule nchini Burundi. Na je wanaofungwa kinyume cha sheria watapataje haki? Mtayarishaji wa makala ni Amida Issa akiwa mjini Bujumbura, Burundi.
Chad inafanya uchaguzi wa rais leo Jumatatu baada ya miaka mitatu ya utawala wa kijeshi. Uchaguzi huo ni wa kwanza kwenye kanda ya Sahel tangu eneo hilo liliposhuhudia wimbi kubwa la mapinduzi ya kijeshi.