Deutsche Welle: Katika siku ya pili ya mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika, Cote d'Ivoire inaumana na Sudan na Burkina Faso inashuka dimbani kupambana na Angola.
Karibu katika matangazo ya asubuhi ya DW Kiswahili
Jumuiya ya kujihami ya NATO yasema wanachama wake hawajatimiza ahadi ya msaada wa silaha kwa Ukraine, mfanyakazi wa zamani wa NSA ahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 21 kwa kujaribu kuifanyia Urusi upelelezi na Togo yapiga kura kuwachagua wabunge baada ya mageuzi ya kikatiba yaliyosababisha mgawanyiko
Raia wa Togo wamepiga kura kuwachagua wabunge baada ya mageuzi ya kikatiba yaliyosababisha mgawanyiko ambao wapinzani wanasema yanampa Rais Faure Gnassingbe mwanya wa kuongeza muda wa kuendelea kushika madaraka