Bunge la Kenya limeupitisha mswada unaoishauri serikali ijiondoe kwenye mkataba wa Roma ulioiunda mahakama ya uhalifu wa kivita ICC iliyoko The Hague
China inafanya luteka ya kijeshi kwa mashambulizi ya makombora na kupeleka ndege za kivita ikiwa ni katika mazoezi yake ya siku mbili dhidi ya Taiwan.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo, yafanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi, lililofanyika katika ikulu ya rais mjini Kinshasa. Rais wa Kenya william Ruto afanya ziara mjini Washington alikokutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden na Kiongozi wa upinzani Uganda Robert Kyagulanyi apinga kuzuwiwa kwa mikutano yao ya kisiasa. Jiunge na Amina Abubakar Mjahid katika Afrika Wiki Hii.
Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ imeitaka Israel kusitisha mara moja mashambulizi yake huko Rafah+++Mawaziri wa Fedha wa kutoka nchi tajiri kiviwanda za kundi la G7, wameanza mkutano wao wa siku mbili nchini Italia kwa shabaha ya kutafuta mpango wa pamoja katika kuipata mkopo Ukraine