Korea Kaskazini imelikataa pendekezo la kufanya mazungumzo na Korea Kusini ili kutuliza hali ya wasiwasi katika eneo hilo la Korea.
Upepo mkali na mvua kubwa yashuhudiwa pwani ya kusini ya Tanzania.I Meli ya kivita ya Iran yavuka Ikweta hadi kizio cha kusini.I Mahakama ya kijeshi yawahukumu kifo askari wanane Kongo.I Rwanda yakanusha shutuma za Marekani kuhusika na shambulizi la Goma.
Iran yasema Meli yake kivita iitwayo Shahid Mahdawi, ikiwa na droni na makombora, kwa mara ya kwanza, imevuka Ikweta hadi Kizio cha Kusini.
Shirika la Ulinzi wa raia la Brazil limesema kuongezeka kwa viwango vya maji katika jimbo la Rio Grande do Sul kulikuwa kukiyafurisha mabwawa na kutishia jiji kuu la Porto Alegre.