Deutsche Welle: Wanamgambo wa jimbo la Darfur wamemchagua Gibril Ibrahim kukamata nafasi ya nduguye Khalil aliyeuliwa Disemba mwaka jana na wanajeshi wa Sudan.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, ameyatolea wito mataifa yanayoisaidia Sudan kusitisha msaada kwa pande zinazozozana nchini humo, akionya kuwa kuna hatari ya mauaji ya kimbari.
Marekani imetaka msaada wa silaha kwa pande zinazohasimiana nchini Sudan kusitishwa, huku ikionya kwamba historia katika eneo la Darfur ambako kulishuhudiwa mauaji ya halaiki miaka 20 iliyopita "inajirudia."
Marekani imezitaka nchi zote zinazopeleka silaha Sudan kusitisha hatua hiyo ikionya kwamba historia inajirudia katika jimbo la Darfur,Magharibi mwa Sudan ambako yaliwahi kushuhudiwa mauaji ya halaiki miaka 20 iliyopita.