Deutsche Welle :Eneo la Tahrir mjini Cairo linapitika tena sasa baada ya maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuondolewa kwa utawala wa Hosni Mubarak.
Waziri wa Afya Uingereza Victoria Atkins, amesema serikali ya nchi hiyo ina mpango wa kuwapeleka nchini Rwanda wahamiaji wapatao 6,000 kwa mwaka huu, baada ya kuchapisha maelezo mapya kuhusu mpango huo wenye utata.
Mhubiri wa kanisa la Good News International, Paul Mackenzie na wenzake 94 hii leo wanafikishwa katika Mahakama Kuu ya Mombasa nchini Kenya kusomewa mashtaka ya jinai.
Wajumbe wa makundi ya wapiganaji wa Kipalestina ya Hamas na Fatah wamekutana kwa mazungumzo mjini Beijing na kutangaza nia yao ya kufikia maridhiano.