Deutsche Welle: Katika mechi za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika hivi leo, Sudan inakwaana na Burkina Faso, wakati Cote d'Ivoire ikitoana jasho na Angola.
Utawala wa kijeshi wa Burkina Faso umevipiga marufuku vyombo vya habari zaidi vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na DW. Hatua hii ni sehemu ya mtindo wa ukandamizaji wa vyombo vya habari.
Marekani itatoa msaada wa karibu dola milioni 55 kushughulikia mzozo mbaya wa kibinadamu nchini Burkina Faso. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu ofisi ya Misaada ya Kitutu ya Marekani, Samantha Power.
Mamlaka ya Burkina Faso imesema imesimamisha kwa wiki mbili matangazo ya BBC na VOA baada ya kuiangazia ripoti iliyodai jeshi la nchi hiyo linatekeleza mauaji ya kiholela.