Viongozi wa Afrika leo wanakutana katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta- Malabo, pamoja na masuala mengine kuujadili mgogoro wa Libya.
Chad inafanya uchaguzi wa rais leo Jumatatu baada ya miaka mitatu ya utawala wa kijeshi. Uchaguzi huo ni wa kwanza kwenye kanda ya Sahel tangu eneo hilo liliposhuhudia wimbi kubwa la mapinduzi ya kijeshi.
Yaliyomo katika taarifa ya habari za ulimwengu kwenye matangazo ya Dw Jioni, ni ziara ya rais wa China Xi Jinping barani Ulaya,na Matumaini ya kufikiwa makubaliano kuhusu vita vya Gaza yafifia nchini Misri.Utasikia pia makala ya maoni mbele ya meza ya duara inayojadili athari za mabadiliko ya tabia nchi Afrika Mashariki.
Mamlaka nchini Kenya zimesema kuwa idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko imeongezeka hadi kufikia watu 228.