Katika mechi za duru ya tano ya Kombe la Klabu Bingwa, leo usiku timu ya ligi kuu ya Ujerumani, Schalke, inamenyana na Steaua Bucharest ya Romania.
Schalke waliamua heri punda afe lakini mzigo ufike na kulazimisha sare katika uga wa nyumbani Veltis Arena na mashabiki walisherehekea sare hiyo kama ushindi wakati timu yao iko kwenye eneo la kushushwa daraja. Dortmund ilikosa huduma za nahodha Marco Reus na kiungo wa kati Julian Brandt.
Nani alisema Bundesliga inatabirika? Hizi ni nyakati za kushangaza katika ligi kuu ya kandanda Ujerumani. Union Berlin wameingia katika kipindi cha mechi za kimataifa wakiwa kileleni mwa Bundesliga
Mshambuliaji wa klabu ya Schalke Sebastian Polter huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa kutokana na jeraha baya alilolipata kwenye goti katika mechi ya kirafiki na FC Zurich ya Uswisi. Jitihada za Schalke kujinasua mkiani mwa Bundesliga zitaathirika vipi? Msikilize Josephat Charo akihojiwa na Naomi William.