1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia Dortmund yatinga fainali Champions League

8 Mei 2024

Klabu ya soka ya Ujerumani ya Borussia Dortmund imetinga fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kupata ushindi mbele ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4fbln
Ufaransa| Champions League| Dortmund
Dortmund wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya PSG. Picha: Christophe Ena/AP Photo/picture alliance

Dortmund iliyokuwa ugeneni katika duru ya pili ya nusu fainali,iliibamiza PSG --klabu ya nyota Kylian Mbappe-- bao 1-0 katika mchezo uliopigwa mjini Paris.

Bao la Dortmund lilifungwa mnamo dakika ya 50 na Mats Hummels aliyepiga kichwa kwa ustadi na kupachika mpira wavuni. Nafasi ya Dortmund kufika fainali ilikuwa wazi baada ya kushinda pia bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wiki iliyopita.

Hiyo itakuwa ni mara ya tatu kwa Dortmund kucheza fainali ya Champions League. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2013 na ilipoteza tonge mkononi kwa kibano cha mabao 2-1 kutoka kwa mahasimu wao, Bayern Munich.

Mwaka huu pia Dortmund wanaweza kukutana fainali na Bayern Munich inayosubiri mchezo wa pili wa nusu fainali dhidi ya Real Madrid utakaopigwa leo usiku.