1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Risasi zarindima nyumbani kwa mwanasiasa wa Kongo Kamerhe

19 Mei 2024

Milio ya risasi imerindima kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kinshasa.

https://p.dw.com/p/4g34O
Vital Kamerhe
Vital KamerhePicha: Reuters/B. Ratner

Ni pale watu wenye silaha waliovalia sare za jeshi walipopambana na walinzi wa mwanasiasa kigogo Vital Kamerhe kwenye makaazi yake yaliko karibu na Ikulu ya nchi hiyo.

Duru kutoka nchini humo zinasema watu watatu wameuwawa kwenye makabiliano hayo. Msemaji wa Kamerhe amearifu kwamba watu hao wenye silaha walivamia makaazi ya mbunge huyo na waziri wa uchumi lakini walidhibitiwa na walinzi wake.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimewatambulisha watu hao kuwa wanajeshi wa Kongo lakini haikufahamika mara moja juu ya iwapo walikwenda kwenye makaazi ya Kamerhe kwa lengo la kumkamata.

Hivi sasa Kamerhe anawania kiti cha spika wa bunge la taifa katika uchaguzi uliopangwa kufanyika jana Jumamosi lakini uliahirishwa kutokana na mivutano ndani ya chama tawala.