1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Armenia na Azerbaijan zakubaliana msingi wa mkataba wa amani

18 Novemba 2023

Armenia na Azerbaijan zimekubaliana kanuni za msingi katika mkataba wa amani baina ya nchi hizo mbili ila bado wanatofautiana kidiplomasia.

https://p.dw.com/p/4Z8OD
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan akizungumza katika bunge la Ulaya Straßburg
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol PashinyanPicha: Frederic MARVAUX/EP

Haya yamesemwa na Waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan.

Kulingana na shirika la habari la Urusi la TASS, Pashinyan amesema kuna hatua zilizopigwa katika mazungumzo yanayoendelea kuhusiana na mkataba wa amani, ingawa amenukuliwa akisema kuwa nchi hizo mbili aghalabu huwa na wakati mgumu kukubaliana kuhusu baadhi ya mambo.

Armenia na Azerbaijan zimezozana kwa miongo kadhaa sasa kutokana na eneo la Nagorno-Karabakh ambalo majeshi ya Azerbaijan yalichukua tena udhibiti wake mwezi Septemba na kupelekea idadi kubwa ya Waarmenia kuondoka.