1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern, Dortmund katika mechi muhimu za Ligi ya Mabingwa

Bruce Amani
29 Aprili 2024

Wiki chache zijazo huenda zikaliweka kandanda la Ujerumani kwenye ramani. Ujerumani inajiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Ulaya katika miezi ya Juni na Julai, huku timu ya taifa ya Ujerumani ikiimarika fomu yake.

https://p.dw.com/p/4fJGb
Bayern Munich wamekuwa na matokeo mazuri katika Ligi ya Mabingwa
Bayern Munich wanalenga kubeba ubingwa wa Ulaya baada ya kuwachia taji la ligiPicha: Odd Andersen/AFP/Getty Images

Wiki chache zijazo huenda zikaliweka kandanda la Ujerumani kwenye ramani. Ujerumani inajiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Ulaya katika miezi ya Juni na Julai, huku timu ya taifa ya Ujerumani ikionekana kuanza kupata fomu nzuri chini ya kocha Julian Nagelsmann.

Lakini kabla ya hapo, Ujerumani huenda ikasherehekea kuwa na bingwa wa Ulaya kwa mara nyingine. Bayern Munich na Borussia Dortmund zinacheza nusu fainali za Ligi ya Mabingwa zinazoanza kesho.

Mara ya kwanza Bayern na Dortmund zilifika nusu fainali za Ligi ya Mabingwa ilikuwa mwaka wa 2013 na zikaenda hadi fainali ya Wembley ambapo Bayern walishinda 2 -1. Na ikumbukwe kuwa fainali ya mwaka huu pia itachezwa katika dimba hilo.

Bayern kesho wanawaalika miamba ya Real Madrid, ambao wanashikilia rekodi ya mataji 14 ya Ulaya. Dortmund watacheza dhidi ya Paris Saint Germain.

Ujerumani haikuwa na mwakilishi katika nusu fainali kwenye misimu mitatu iliyopita. Katika mashindano ya 2019-2020, ilikuwa timu mbili _ Bayern na Leipzig na kisha Bayern wakabeba ubingwa. Msimu huu, Bayern na Dortmund zimekuwa na matokeo mazirind zimekuwa na matokeo mazuri katika mashindano ya Ulaya huku zikiwa na hali ngumu katika ligi ya nyumbani.

afp, dpa, reuters, ap