1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yasema Beijing inapendelea ushirikiano na Ujerumani

20 Juni 2023

Waziri Mkuu wa China Li Qiang aliye ziarani nchini Ujerumani amesema Beijing inalenga kutumia mashauriano ya ngazi ya kiserikali na Ujerumani kutanua ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili na kutatua tofauti zilizopo.

https://p.dw.com/p/4Sntd
Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz jijini Berlin,Ujerumani
Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz jijini Berlin,UjerumaniPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Li Qiang ameyasema hayo mjini Berlin muda mfupi baada ya kupokelewa na rais Frank-Walter Steinmeier kuanza ziara rasmi nchini Ujerumani.

Qiang ambaye ziara yake nchini Ujerumanni ni kwanza tangu alipoteueliwa kushika wadhifa huo amesema anatumai kuona ishara dhahiri za kuwepo sekta imara ya viwanda kimataifa pamoja na amani duniani.

Amesisitiza kwamba China iko tayari kufanya kazi pamoja na Ujerumani kuzika tofauti za kimtazamo zilizopo na kuimarisha mahusiano.

Hapo jana jioni Qiang alikaribishwa dhifa ya chakula cha jioni na kansela Olaf Scholz na hii leo anatarajiwa kushiriki awamu ya saba ya mashauriano ya kiserikali kati ya China na Ujerumani.