1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yasema mazungumzo na mkuu wa IAEA yalikuwa mazuri

7 Mei 2024

Mazungumzo kati ya maafisa wa Iran na mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia IAEA, Rafael Grossi yamekuwa na matokeo chanya.

https://p.dw.com/p/4fayo
Rafael Grossi na Mohammad Eslami in Isfahan
Mkuu wa IAEA Rafael Grossi alifanya mazungumzo mjini Tehran na Mohammad EslamiPicha: Tasnim

Mazungumzo kati ya maafisa wa Iran na mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia IAEA, Rafael Grossi yamekuwa na matokeo chanya. Hayo yameelezwa hivi leo na Mohammad Eslami ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha masuala ya nyuklia nchini Iran.

Mazungumzo hayo yalifanyika katika mji wa Isfahan baada ya Grossi kuanza ziara rasmi nchini humo hapo Jumatatu ili kutathmini programu za nyuklia za Iran, akitumai pia kuimarisha usimamizi wa Shirika la IAEA dhidi ya programu hiyo baada ya vuta ni kuvute ya muda mrefu.

Lakini wachambuzi na wanadiplomasia wanasema Grossi ana uwezo mdogo wa kuishinikiza Iran na lazima awe mwangalifu na ahadi tupu zinazoweza kutolewa na serikali mjini Tehran ambayo imekuwa ikishtutumiwa kurutubisha madini ya urani kwa lengo la kuunda silaha za nyuklia.