1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Jengo laporomoka Afrika Kusini na kuuwa watu watano

7 Mei 2024

Jengo kubwa la ghorofa ambalo lilikuwa bado kwenye ujenzi limeporomoka katika mji wa George, nchini Afrika Kusini na kusababisha vifo vya watu watano.

https://p.dw.com/p/4fZuo
Jengo laporomoka
Mikasa ya kuporomoka majengo Afrika Kusini sio ya kawaidaPicha: Tarekuzzaman

Jengo kubwa la ghorofa ambalo lilikuwa bado kwenye ujenzi limeporomoka katika mji wa George, nchini Afrika Kusini na kusababisha vifo vya watu watano huku wengine zaidi ya 50 wakiwa wamenaswa chini ya vifusi.

Mamlaka nchini humo zimesema mapema leo kuwa watu 24 wameokolewa lakini wengine wapatao 51 bado hawajapatikana. Uongozi wa jiji hilo la pwani umesema kuwa mafundi 75 walikuwa katika jengo hilo wakati lilipoporomoka jana alasiri lakini wamefanikiwa kuzungumza na watu 11 walionaswa chini ya vifusi.

Mji wa George wenye wakazi 160,000 unapatikana katika eneo linalopendwa mno na watalii katika ukanda wa pwani ya kusini mwa nchi hiyo. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametolea salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza jamaa zao na kuamuru kufanyike uchunguzi wa kina.