1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya ECCAS yaisimamisha uanachama Gabon

Josephat Charo
5 Septemba 2023

Jumuiya ya uchumi ya Afrika ya Kati imesitisha uanachama wa Gabon kwa sababu ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Agositi 30 ambapo rais Ali Bongo aliondolewa madarakani.

https://p.dw.com/p/4VxNv
Äquatorialguinea Präsident Teodoro Obiang Nguema Mbasogo
Picha: Ju Peng/Xinhua/imago images

Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS imeamua kusimamisha unachama wa Gabon kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 30 yaliyomuondoa madarakani rais Ali Bongo. Jumuiya ya ECCAS imetoa taarifa hiyo baada ya kikao chake kilichofanyika jana Jumatatu katika mji mkuu wa nchi jirani ya Guinea ya Ikweta, Malabo.

Rais wa Guinea ya Ikweta, Teodoro Obiand Nguema amesema Gabon ni kitisho kwa amani, usalama na uthabiti katika nchi nyingine wanachama wa jumuiya ya ECCAS.

Hatua hii inafuatia kuapishwa hapo jana kwa jenerali Brice Oligui Nguema aliyeongoza mapinduzi ya Gabon kama rais wa mpito, akiahidi uchaguzi huru, wazi na wa kuaminika kwa lengo la kurejesha utawala wa kiraia lakini hakutaja tarehe maalumu.