1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukizi ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania

26 Aprili 2024

Tanzania inaadhimisha Ijumaa miaka 60 ya muungano ulioasisiwa mnamo Aprili 26 mwaka 1964 kuziunganisha dola mbili iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

https://p.dw.com/p/4fD7g
Tansania | Detailaufnahme der Tansania Flagge vor blauem Himmel
Picha: Valerio Rosati/Zoonar/picture alliance

Hoja kadhaa za Muungano zimekuwa zikitolewa na wengi wakiamini kuwa hazijapatiwa suluhu na hoja hizo kupewa majina mbalimbali kama kero au changamoto.

Upande wa serikali zote mbili  zimekuwa kila mara zikitangaza kuwa ni Muungano wa Tanzania ni wa kupigiwa mfano duniani huku wakieleza kuwa upo salama na kuimarika zaidi tofauti na maoni ya wananchi wa pande mbili hizo.

Hoja ya Usalama wa Muungano haionekani ina uzito kwa wakosoaji wake hasa wazanzibari ambao wanadai kuna tatizo ndani ya muundo na kwamba lengo lake kuu ikiwa ni kuibana Zanzibar.

Maoni mseto kuhusu muungano

Wakosoaji hao wanadai Muungano huo unapaswa ubadilike pia kwenye haki za washirika wa Muungano kama ilivyo Pendekeza Tume ya Jaji Warioba ya kukusanya maoni ya kuandika katiba mpya mwaka 2014 mapendekezo ambayo yaliondolewa na Bunge la Katiba. Mojawapo ilikuwa ni pendekezo la muundo wa serikali tatu badala ya mbili zilizopo sasa.

Vijana ambao wamezaliwa baada ya Muungano wanaona Muungano huu ni mzuri na unapaswa kuendelezwa. Wadadisi wengi wanaamini ubora wa Muungano ni ule ambao utakuwa ni wa haki, uwazi na ushirika na kutekelezwa kwa dhati matakwa ya katiba.

Maoni ya wazee wanaona wajibu wa wasimaizi wakuu wa Muungano ni kuhakishisha kuwa mambo yaliotajwa katika Katiba kwa mfano kuundwa mfuko wa Pamoja wa Fedha na mahakama ya Katiba kama suluhu ya changamoto kubwa zinazoukabili muungano huo.