1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron: Ulinzi wa Ulaya unapaswa kuwa zaidi ya NATO

Tatu Karema
29 Aprili 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa silaha za nyuklia za Ufaransa zinapaswa kuwa sehemu ya mjadala wa ulinzi wa Ulaya

https://p.dw.com/p/4fHOQ
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba kuhusu Ulaya katika chuo kikuu cha Sorbonne mnamo Aprili 25, 2024
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Christophe Petit Tesson/AP Photo/picture alliance

Wakati wa mahojiano na EBRA, kundi la magazeti ya kikanda ya mashariki mwa Ufaransa, Macron alisema kuwa ulinzi thabiti wa Ulaya unapaswa kuwa zaidi ya ulinzi unaotolewa na jumuiya ya kujihami ya NATO.

Soma pia:Mkuu wa NATO aonya EU haiwezi kuilinda Ulaya peke yake

Macron ameongeza kuwa hatua hiyo huenda ikamaanisha matumizi ya ngao za kuzuia makombora, lakini pia kuhakikisha kwamba wanazuia matumizi ya silaha za nyuklia.

Macron yuko tayari kutoa mwelekeo wa Ulaya kwenye matumizi ya silaha ya nyuklia

Kuhusu silaha za nyuklia, wakati utaratibu wa Ufaransa kufikia sasa umekuwa kuzitumia wakati  maslahi muhimu ya nchi hiyo yanakabiliwa na vitisho, Macron amesema yuko tayari kutoa mwelekeo zaidi wa Ulaya kwenye maslahi hayo.