1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaBrazil

Mafuriko yaua watu 75 na kujeruhi wengine 155 Brazil

6 Mei 2024

Mafuriko makubwa yaliyolikumba jimbo la kusini mwa Brazil la Rio Grande do Sul yamesababisha vifo vya watu 75 na wengine 103 wamepotea hu juhudi za kuwatafuta zinaendelea.

https://p.dw.com/p/4fWy6
Mafuriko yaliyoikumba Brazil.
Mafuriko yaliyoikumba Brazil.Picha: Amanda Perobelli/REUTERS

Hayo yameelezwa mamlaka za jimbo hilo jana Jumapili ambazo pia zimearifu watu wengine wasiopungua 155 wamejeruhiwa huku janga hilo limesababisha vilevile zaidi ya watu 88,000 kuzikimbia nyumba zao.

Kati yao, watu wapatao 16,000 wanahifadhiwa kwenye majengo ya shule, kumbi za mazoezi na makaazi ya muda. Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku saba yamesababisha maporomoko ya udongo, yamesomba barabara na kuvunja madaraja ya jimbo hilo.

Hapo jana Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil alilitembelea jimbo hilo wa mara ya pili akiwa ameongozana na mawaziri kukagua uharibifu uliotokea. Alizunguka kwa helikopta kwenye wilaya ya Porto Alerge iliyoathiriwa zaidi na janga hilo na kutoa ahadi ya msaada wa serikali kuu.