1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Makundi ya makabila yaliyojihami kwa silaha nchini Myanmar

Tatu Karema
16 Desemba 2023

Makundi ya makabila madogo yaliyojihami kwa silaha nchini Myanmar, yanayopigana na utawala wa kijeshi nchini humo, yamesema kuwa yameliteka eneo la kibiashara la Namhsan katika jimbo la Shan

https://p.dw.com/p/4aF1I
Wapiganaji wa jeshi la Myanmar National Democratic Alliance  katika mji wa Kunlong jimboni Shan
Wapiganaji wa jeshi la Myanmar National Democratic Alliance Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Makundi ya makabila madogo yaliyojihami kwa silaha nchini Myanmar, yanayopigana na utawala wa kijeshi nchini humo, yamesema  kuwa yameliteka eneo la kibiashara la Namhsan katika jimbo la Shan, siku chache baada ya China kusema kuwa imesimamia makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano.

Jeshi la ukombozi la Ta'ang National (TNLA) limesema jana kuwa limeteka eneo hilo la Namhsan baada ya kuanzisha mashambulizi katika eneo hilo zaidi ya wiki mbili zilizopita. Brigedia jenerali Tar Bhone Kyaw wa TNLA, amethibitisha kuliteka eneo la Namhsan kwa shirika la habari la AFP.

Soma pia;Takriban Watu 50,000 wayakimbia makwao kufuatia mapigano kaskazini mwa Myanmar: UN

TNLA ilichapisha kanda ya video katika mtandao wa facebook ikionesha viongozi wake wakifanya ziara mjini humo na kuzungumza na wanajeshi wa Myanmar waliochukuliwa mateka.

Msemaji wa jeshi la Myanmar Brigedia Jenarali Zaw Min Tun jana alikiambia kituo cha televisheni cha serikali MRTV kwamba mapigano yanaendelea katika eneo hilo la Namhsan.