1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Mawaziri wa Japan na China wakutana Beijing

2 Aprili 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Japan Yoshimasa Hayashi amesema ameitolea wito Beijing kumuwachia huru mapema raia wa Japan aliyekamatwa nchini China.

https://p.dw.com/p/4PbW3
China Peking | Japanischer Außenminister Yoshimasa Hayashi trifft Qin Gang
Picha: Kyodo News/IMAGO

Ameyasema hayo katika mkutano wa leo na mwanadiplomasia mkuu wa China Qin Gang. Hayashi anazuru China na alikutana na mwenzake Qin, ikiwa ni ziara ya kwanza mjini Beijing kufanywa na waziri wa mambo ya kigeni wa serikali ya Japan katika zaidi ya miaka mitatu, wakati nchi hizo mbili zikitafuta maelewano wakati kukiwa na ongezeko la mivutano ya kikanda.

Aliongeza kuwa Japan inatafuta uwazi kuhusu utaratibu wa kisheria wa kuwekwa watu kizuizini na kuiomba China kutengeneza mazingira ya haki na salama ya kibiashara lakini hakufafanua kuhusu jibu la China.

Hayashi pia alielezea wasiwasi mkubwa wa Japan kuhusu kuongezeka kwa shughuli za kijeshi za China, ikiwemo ukaribu wake na Urusi na uwepo wake katika Bahari ya Mashariki ya China.