1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Nigeria yasema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa

18 Januari 2023

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria amesema nchi hiyo haitaahirisha uchaguzi mkuu wa mwezi ujao, licha ya wasiwasi juu ya kuzorota kwa usalama na mashambulizi dhidi ya maafisa wa uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4MMH0
Nigeria Reis-Pyramide gegen die Hungersnot im Land
Picha: Koula Sulaimon/AFP

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria amesema nchi hiyo haitaahirisha uchaguzi mkuu wa mwezi ujao, licha ya wasiwasi juu ya kuzorota kwa usalama na mashambulizi dhidi ya maafisa wa uchaguzi.

Akizungumza mjini London, afisa huyo, Mahmood Yakubu amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imejiandaa vyema kuendesha uchaguzi katika taifa hilo lenye wakaazi wengi zaidi barani Afrika pamoja na changamoto zilizopo.

Raia wa Nigeria watamchagua rais mpya tarehe 25 Februari, atakayechukua nafasi ya rais wa sasa Muhammadu Buhari ambaye muhula wake wa pili na wa mwisho umemalizika. Seneti Nigeria yabadili sheria ya matokeo ya uchaguzi

Nchi hiyo inao wakaazi wapatao milioni 200 na uchumi imara zaidi barani Afrika, na mapambano yake dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali za kiislamu yanatazamwa na wengi kama kigezo muhimu kwa utangamano wa kikanda.