1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aamuru mazoezi ya silaha za nyuklia karibu na Ukraine

6 Mei 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza kufanyika kwa luteka za kijeshi zikihusisha silaha za nyuklia karibu na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4fYg6
Urusi | Rais Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Kremlin.ru/REUTERS

Kulingana na Rais Putin, hatua hiyo ni ya kushughulikia kile alichokiita ''kitisho'' cha nchi za Magharibi cha kupeleka vikosi vya Jumuiya ya kujihami NATO nchini Ukraine.

Wizara ya ulinzi ya Urusi haikutoa maelezo zaidi kuhusu tarehe ya kuanza kwa mazoezi hayo, lakini yatajumuisha vikosi vya wanaanga, majini na vile vilivyoko karibu na Ukraine. 

Tangazo hilo limetolewa mnamo wakati vikosi vya Urusi vikidai kukamata vijiji viwili katika mikoa inayokabailiwa na vita ya Donetsk na Kharkiv mashariki mwa Ukraine.

Putin amezidisha kauli zake kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia tangu alipoivamia Ukraine mwaka 2022. Mnamo mwezi Februari Putin alinukuliwa akionya kwamba kuna kitisho halisi cha vita vya nyuklia.