1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Rais Putin wa Urusi aapishwa kuongoza kwa muhula wa tano

7 Mei 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameapishwa na kuanza rasmi muhula mwingine wa miaka sita madarakani baada ya kupata ushindi wa kishindo wa asilimia 87 ya kura.

https://p.dw.com/p/4fZvx
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Putin ameapishwa kuwa rais wa Urusi kwa muhula wake wa tano baada ya kushinda uchaguzi uliosusiwa na upinzaniPicha: Kremlin.ru via REUTERS

Putin mwenye umri wa miaka 71 na ambaye ametawala siasa za urusi kwa miaka 24, amekula kiapo katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, na kuhudhuriwa na wanasiasa waandamizi wa Urusi, pamoja na wageni waalikwa ambao ni viongozi wenye vyeo vya juu.

Soma pia: Tume ya uchaguzi yapigilia msumari ushindi wa Putin

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Putin amesema mifumo ya nchi yake ni lazima iwe tayari kukabiliana na kitisho cha aina yoyote lakini akasisitiza kuwa, Urusi haitositisha mazungumzo na mataifa ya Magharibi lakini akazitaka nchi hizo kuwa na maamuzi.

Soma pia: Putin ahutubia umati wa Red Square baada ya ushindi mnono

Ili kusalia madarakani, Putin aliifanyia marekebisho katiba ya Urusi miaka michache iliyopita. Mabadiliko hayo yatamuwezesha Putin baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2030, kuruhusiwa kugombea tena na kusalia madarakani hadi mwaka 2036, atakapokuwa na umri wa miaka 83.