1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSudan Kusini

Sudan Kusini yafuta kodi na ada kwa bidhaa za misaada

5 Mei 2024

Sudan Kusini imetangaza kuachana na uamuzi wake wa mwezi Februari, wa kutoza kodi kwenye bidhaa ya mafuta, ada za gharama za ufuatiliaji wa mizigo kielektroniki, pamoja na ada za kusindikiza mizigo hiyo.

https://p.dw.com/p/4fWC9
Sudan Kusini | Mbegu za nafaka
Mwanamke akionesha mbegu za nafaka huko Bentiu, Sudan Kusini: 28.11.2023Picha: Luke Dray/Getty Images

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia wito wa Umoja wa Mataifa baada ya kusitishwa kwa utoaji wa tani kadhaa za misaada ya chakula huku maelfu ya watu katika nchi hiyo masikini wakitegemea misaada kutoka nje.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, inakadiriwa kuwa watu milioni 9 kati ya milioni 12.5 wa Sudan Kusini wanahitaji ulinzi na usaidizi wa kibinadamu.

Soma pia: Zaidi ya watu milioni 7 kukabiliwa na njaa Sudan Kusini

Nchi hiyo imeshuhudia pia ongezeko la watu kutokana na wakimbizi kutoka nchi jirani ya Sudan, jambo ambalo linazidisha ugumu katika masuala ya utoaji misaada ya kibinaadamu.