1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kupambana na ubaguzi ni swala la haki

21 Machi 2023

Ushiriki wa makundi yote ya kijamii haimaanishi kuwa watoa maamuzi wa awali wananyimwa fursa bali hii ni haki ya kidemokrasia anasema mwandishi wa DW Sheila Mysorekar.

https://p.dw.com/p/4OyYA
Anti Rassismus Konferenz 2001 in Durban Demonstration
Picha: picture-alliance / dpa

Katika bara la Ulaya, swala la kuharamisha ubaguzi wa rangi linapaswa kuwa ni swala lililotekelezwa zamani. Lakini kwa bahati mbaya hali sivyo ilivyo. Katika nchi kadhaa za Ulaya, vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia na vya kibaguzi vinawakilishwa katika mabunge au hata kwenye serikali.

Uadui unaolenga makundi ya watu, unaojumuisha ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya Wayahudi, ubaguzi dhidi ya Waislamu, chuki dhidi ya wanawake, au chuki kwa kuzingatia jinsia na kuwachukia watu wengine, kwa bahati mbaya mambo haya bado ni sehemu muhimu ya jamii nyingi za Ulaya.

Vijana wa Ujerumani wanahamasisha watu kuishi pamoja kwa amani, kujifunza na kushirikiana katika kupinga ubaguzi.
Vijana wa Ujerumani wanahamasisha watu kuishi pamoja kwa amani, kujifunza na kushirikiana katika kupinga ubaguzi.Picha: Becker&Bredel/imago images

Hakuna mahali jambo hili linajionesha zaidi kuliko katika hatua za kuifunga mipaka ya Ulaya kwa wale wanaotafuta hifadhi kutoka nchi za Afrika, Asia na nchi za Kiarabu. Kwa watu hao haiwezekani tena kuingia Ulaya bila ya kwanza kuzuiliwa huko waliko kabla ya kuomba hifadhi jambo ambalo limeidhinishwa rasmi katika sheria za kimataifa licha ya kuwa kuomba hifadhi ni mojawapo ya haki za kimsingi kwa watu wote.

Kutokana na hali hiyo, watu wapatao 350 wamezama katika bahari ya Mediterania tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Watu hao wanaokimbia vita na ukandamizaji, wanaingia kwenye safari za hatari kwa kupanda boti ndogo za mpira kwa matumaini ya kufikia ufuo wa bahari za Ulaya kwa ajili ya kupata makazi salama.

Vifo kwenye Bahari ya Mediterania

Kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), takriban watu 2,406 walikufa kwenye safari hizo katika Bahari ya Mediterania mnamo mwaka 2022, ikilinganishwa na zaidi ya watu 3,000 waliopoteza maisha mwaka uliotangulia.

Ujerumani ndio nchi pekee barani Ulaya ambayo imewachukua wakimbizi wengi zaidi, ikiwa na zaidi ya wakimbizi milioni moja kutoka Syria na Ukraine. Huku nchi nyingine, kama vile Hungary au Uingereza, zinajivunia kuipindua haki ya kupata hifadhi katika ardhi zao.

Kwa jumla ubaguzi umepata sura mpya kwani sasa mazungumzo sio tena ya rangi ya mtu bali ni tamaduni ambazo inasemekana hazilingani na maadili ya Magharibi. Hili halitumiki tu kwa wakimbizi bali pia kwa watu kutoka kwenye familia za kimataifa ambao wameishi Ulaya kwa vizazi na vizazi.

Wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali kwenye maandamano ya kupinga ubaguzi.
Wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali kwenye maandamano ya kupinga ubaguzi.Picha: picture-alliance / dpa

Wanakandamizwa kwa kudaiwa kuwa hawako tayari kujumuika, dini zao hazina mitazamo ya kisasa, elimu yao ni duni sana. Hatua ya mwisho kuhusiana na ubaguzi wa kimuundo mara nyingi haieleweki vyema hata na wanasiasa.

Hata hivyo, uthibitisho wote huu unahojiwa mara kwa mara lakini kwa lengo la kuufunika mjadala wa kweli kuhusu ubaguzi na maswali juu ya mamlaka. Kwa muda mrefu sana hatuzungumzi juu ya mashaka halisi ya walio wachache. Lakini hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa yaani ushiriki, heshima na haki.

Ingawa kuna watu wengi na mashirika nchini Ujerumani ambayo yanaendeleza vita dhidi ya ubaguzi na kati ya wanaharakati hao wengi ni Wajerumani wanotoka katika jamii za wahamiaji. La muhimu kutilia maani ni kwamba ukosoaji si dhambi, bali ni ishara ya jamii hai ya kidemokrasia ambapo kila mtu anashiriki katika majadiliano.