1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda kurejesha nyumbani mabaki ya mashahidi wawili

6 Mei 2024

Uganda itarejesha nyumbani mabaki ya mashahidi wawili wa Uganda ambao walinyongwa zaidi ya karne moja iliyopita kwa kukataa kuukana Ukristo.

https://p.dw.com/p/4fXcN
Uganda | Kampala
Mifupa ya mashahidi wawili hao inatarajiwa kurejeshwa Uganda mwezi SeptembaPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP/Getty Images

Waumini 22 wa Kikatoliki na 23 wa madhehebu ya Anglikana walinyongwa, wengi wakiwa ni vijana wa kiume kati ya mwaka 1885 na 1886 kwa amri ya aliyekuwa mfalme wa himaya ya Buganda, ambayo sasa ni sehemu ya Uganda.

Kiongozi huyo alikuwa na hofu juu ya kuongezeka kwa ushawishi wa dini ya Kikristo.

Wote waliuawa kikatili, wengi wao wakichomwa moto wakiwa hai na wengine kuchomwa visu au mikuki.

Shirika la Kimishionari la White Fathers lilipeleka mabaki ya mashahidi wawili huko Roma, Italia ambako walitangazwa kuwa watakatifu.

Mifupa ya wawili hao inatarajiwa kurejeshwa Uganda mwezi Septemba na itawekwa kwa ajili ya maonesho katika Chuo Kikuu cha Mashahidi wa Uganda.