1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ukraine: Hali ni mbaya katika mstari wa mbele wa vita

Tatu Karema
29 Aprili 2024

Kiongozi wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrsky amekiri jana kwamba hali ya nchi hiyo kwenye uwanja wa vita imezidi kuwa mbaya baada ya vikosi vya Urusi kuteka kijiji kingine cha mashariki

https://p.dw.com/p/4fHNY
Wanajeshi wa Ukraine washambulia shabaha za Urusi huku wakisubiri msaada wa silaha kwenye mstari wa mbele wa vita vyake na Urusi vinavyoendelea Donetsk, mnamo Desemba 28, 2023
Wanajeshi wa Ukraine washambulia shabaha za UrusiPicha: Elif Kizil/Anadolu/picture alliance

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, Syrsky amesema kuwa hali katika mstari wa mbele wa vita imezidi kuwa mbaya na kwamba katika baadhi ya maeneo, vikosi vya Urusi vilipata ufanisi wa kimbinu na kwingineko, vikosi vya nchi yake viliweza kuboresha nafasi yake ya kimbinu.

Moscow yadai kuchukuwa udhibiti wa mji wa Novobakhmutivka 

Mapema Jumapili, waziri wa ulinzi wa Urusi alidai kuwa vikosi vyake vimeuteka mji wa Novobakhmutivka katika eneo la Donetsk ulioko umbali wa kilomita 10 Kaskazini mwa mji wa Avdiivka, vilivyouteka mwezi Februari.   

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa mkutano na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Riga nchini Latvia mnamo Januari 11,2024
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Gints Ivuskans/AFP

Tathmini kali ya hali inayowakabili wanajeshi wa Ukraine inakuja mwishoni mwa wiki ya heka heka nyingi kwa nchi hiyo.

Marekani yaidhinisha msaada kwa Ukraine

Hatimaye Marekani iliidhinisha msaada wa kifedha wa dola bilioni 61 baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya kisiasa, kwa ununuzi wa silaha zinazohitajika na wanajeshi wa Ukrainekatika mapambano yake dhidi ya Urusi.