1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yafanya mashambulizi makubwa nchini Ukraine

Tatu Karema
27 Aprili 2024

Watu wawili wamejeruhiwa baada ya Urusi kufanya mashambulizi makubwa ya usiku kucha na kuilenga miundombinu ya nishati nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4fFba
Ukraine | Mashambulizi ya Ukraine huko Kharkiv
Uharibifu uliotokana na mashambulizi ya anga ya Urusi katika hospitali huko KharkivPicha: Yakiv Liashenko/AP Photo/picture alliance

Taarifa hii ni kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo. Jeshi la Ukraine limesema Urusi ilifyetua makombora 34 ambapo 21 kati yao yalidunguliwa.

Waziri wa nishati wa nchi hiyo German Galushchenko amesema mashambulizi hayo yamelenga vituo vya nishati  katika maeneo matatu huku kampuni moja kubwa ya kutengeneza umeme  DTEK ikiongeza kuwa mitambo yake minne ya kufua umeme pia imeharibiwa vibaya.

Katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Galushchenko amesema kuwa kwa mara nyingine tena, adui amelenga miundo mbinu ya nishati hasa katika maeneo ya Dnipropetrovsk, Ivano-Frankivsk, na Lviv.