1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Maandamano yanayopinga kubanwa kwa uhuru wa habari Georgia

Amina Mjahid
1 Mei 2024

Watu kadhaa wamekamatwa nchini Georgia, baada ya polisi katika mji mkuu Tbilis kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

https://p.dw.com/p/4fOvh
Georgien Demo gegen das Gesetz über "ausländische Agenten"
Picha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Wizara ya mambo ya ndani ya Georgia imesema watu 63 wamekamatwa kwa kushiriki maandamano hayo. Levan Khabeishvili, mbunge wa upinzani nchini humo alituma picha yake katika mtandao wake wa kijamii ukionyesha uso wake uliojaa damu na kujeruhiwa vibaya huku wanachama wa chama chake wakidai ameshambuliwa na maafisa wa usalama.

Msuada huo unataka vyombo vya habari na mashirika ambayo sio ya kibiashara yanayopokea zaidi ya asilimia 20 ya ufadhili wao kutoka nje yajisajili kwanza  kama mashirika yanayofuatilia na kuendeleza masilahi ya dola ya kigeni.