1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Wachad wapiga kura kuhitimisha utawala wa kijeshi

6 Mei 2024

Wachad wameanza kupiga kura Jumatatu katika uchaguzi unaotazamiwa kuhitimisha utawala wa kijeshi, lakini ambao umepuuzwa na wapinzani wa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby kufuatia ukandamizaji.

https://p.dw.com/p/4fXPf
Chad | Uchaguzi wa rais 2024 | Wapiga kura mjini N’djamena
Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru au wa haki kwani mpinzani mkuu wa Deby ameuawa na wengine kupigwa marufuku kugombea.Picha: Desire Danga Essigue/REUTERS

Wapiga kura nchini Chad wataamua Jumatatu ikiwa watanue miongo kadhaa ya utawala wa familia ya Deby katika mojawapo ya taifa maskini zaidi duniani ambalo pia limekuwa na umuhimu katika mapambano dhidi ya wapiganaji wenye misimamo mikali katika eneo la Sahel.

Deby anachuana na Success Masra ambaye alikuwa waziri wake mkuu, lakini anatazamwa na wakosoaji kuwa ni kibaraka bila ya kuwepo na wapinzani wengine wakubwa.

Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru au wa haki kwani mpinzani mkuu wa Deby ameuawa na wengine kupigwa marufuku kugombea.