1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Watu 24 wapoteza maisha baada ya bwawa kupasuka Kenya

29 Aprili 2024

Takriban watu 42 wamefariki baada ya bwawa la Kijabe kuvunja kingo zake katika eneo la Mahi-Mahiu nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/4fI8L
Janga la mafuriko Kenya
Hivi karibuni Kenya ilikumbwa na janga la mafuriko. Makumi ya watu walikufa na wengi wakapoteza makaazi.Picha: LUIS TATO/AFP/Getty Images

Kulingana na gavana wa kaunti ya Nakuru Susan Kihika, idadi hiyo ni makadirio. Miili zaidi inahofiwa kukwama kwenye tope wakati shughuli za uokoaji zikiendelea.

Bwawa hilo linakiswa kuvunja kingo zake mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya kujaa maji ya  mvua kubwa inayozidi kunyesha.

Maji hayo yalisambaa kwenye mitaa iliyo karibu na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa. Aidha maji hayo yameharibu barabara kuu ya Nairobi- Nakuru na kuyasomba magari ya uchukuzi.

Magari matano ya uchukuzi yalisombwa na maji likiwemo basi lililokuwa na watu 60, hata hivyo hatma ya abiria hao haijulikani.

Kufuatia hali hiyo serikali ya Kenya imeahirisha ratiba ya kufungua shule baada ya likizo kote nchini hadi tarehe sita mwezi ujao. Shule zilitarajiwa kufunguliwa leo.