1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yatala data za ugonjwa hatari wa kupumua

Saumu Mwasimba
23 Novemba 2023

Shirika la afya duniani WHO limeiomba China data kuhusu ugonjwa wa tatizo la kupumuwa unaosambaa katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo. Shirika hilo limetoa wito kuchukuwa hatua za kupunguza kitisho cha maambukizi.

https://p.dw.com/p/4ZLke

WHO imefahamisha kwamba eneo la Kaskazini mwa China limeripoti  ongezeko la maambukizi ya kile kinachoonekana kama homa ya mafua, tangu katikati ya mwezi Oktoba, ikilinganishwa na  miaka mitatu iliyopita katika kipindi kama hicho. Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano, shirika la afya duniani limeitaka China kutowa taarifa ya ufafanuzi zaidi kuhusu ongezeko la magonjwa ya kupumuwa pamoja na homa ya mapafu-Pneumonia kwa watoto.Wiki iliyopita tume ya kitaifa kuhusu masuala ya afya ya China iliwaambia waandishi habari kwamba kuongezeka kwa magonjwa hayo kumetokana na hatua ya kuondolewa vizingiti vya kuzuia kusambaa ugonjwa wa Uviko -19 pamoja na usambaaji wa virusi vinavyosababisha mafua na maambukizi ya bakteria.