1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky atoa ombi la msaada wa mifumo ya ulinzi wa anga

Tatu Karema
27 Aprili 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa ombi jipya la msaada wa mifumo ya ulinzi wa anga baada ya mashambulizi ya usiku kucha ya Urusi dhidi ya miundombinu yake ya nishati

https://p.dw.com/p/4fG2b
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa mkutano na wanahabari mjini Riga, Latvia mnamo Januari 11, 2024
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Gints Ivuskans/AFP

Zelensky amesema Ukraine inahitaji idadi ya kutosha ya mifumo hiyo ya ulinzi wa anga pamoja na silaha nyingine ili kulinda miji yake na kupata ushindi katika mstari wa mbele wa vita.

Soma pia:Ukraine yaishukuru Marekani kwa msaada wa Kijeshi

Rais huyo ameongeza kuwa kila wakati ni lazima ugaidi ushindwe na kwamba yeyote anayelisaidia taifa la Ukraine dhidi ya ugaidi wa Urusi ni mtetezi wa kweli wa haki.

Urusi yaharibu mitambo ya kufua umeme

Matamshi ya Zelensky yanajiri wakati ambapo mapema leo, waziri wa nishati wa nchi hiyo German Galushchenko amesema mashambulizi ya Urusi yamelenga miundombinu ya nishati katika maeneo matatu huku kampuni moja kubwa ya kutengeneza umeme  DTEK ikiongeza kuwa mitambo yake minne ya kufua umeme imeharibiwa vibaya.